The House of Favourite Newspapers

Saido Njiani Kusepa Yanga

0

IMEFAHAMIKA kuwa nyota Mrundi wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, yupo njiani kuondoka ndani ya kikosi hichobaada ya kupata ofa kadhaa nje ya nchi ikiwemo klabu za Afrika na Uarabuni.


Nyota huyu ambaye
anamaliza mkataba wake na Yanga msimu huu, amekuwa tegemeo kwenye kikosi hicho hasa linapokuja suala la mipira iliyokufa.

 


Mtu wa karibu na nyota
huyo, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Mkataba wa Saido na Yanga unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na mpaka sasa ana ofa nyingi nje ya Tanzania zikiwemo ndani ya Afrika na Uarabuni.


“Kama Yanga
wakiendelea kukaa kimya, basi tunaweza kumuona mchezaji akiondoka hata kipindi hiki cha
dirisha dogo au akasubiri
hadi mkataba wake ukimalizika.”


Alipotafutwa Saido
kuzungumzia hilo, alisema: “Kwa sasa si wakati sahihi kuzungumzia masuala hayo.”

STORI: CAREEN OSCAR, DAR

Leave A Reply