
IMEFAHAMIKA kuwa, mapema wiki ijayo, Klabu ya Simba, inatarajiwa kushusha vifaa viwili vya kimataifa ambapo kwa sasa wapo navyo kwenye mazungumzo. Vifaa hivyo ni viungo washambuliaji, Michael Babatunde raia wa Nigeria na Mkenya, Harrison Mwenda.
Babatunde aliyewahi kucheza Wydad Casablanca na Raja Casablanca, kwa sasa ni mchezaji huru
tangu Agosti Mosi, 2021, kama ilivyo kwa Mwenda aliyekuwa akicheza AFC

Leopard ya Kenya na kumaliza mkataba wake Agosti 14, 2021. Mtoa taarifa hizo alisema kuwa, wachezaji hao wapo
kwenye mazungumzo na Simba na kama mambo yakienda vizuri, Januari 4, mwaka huu watatua hapa nchini kusaini mkataba.
“Mazungumzo yameanza kwa kasi ili kukimbizana na muda, kama yakienda vizuri, basi Januari 4, wote
wawili watatua hapa nchini kumalizana kabisa,” kilisema chanzo.
Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alipoulizwa kuhusiana na usajili wa klabu hiyo na taarifa za kufanya
mazungumzo na wachezaji hao, alisema: “Kwa sasa tunayafanyia kazi matakwa ya Kocha (Pablo Franco) na
muda sio mrefu tutawaambia kuwa ni nani tunaachana naye na nani anaingia kikosini.”
Mbali na nyota hao, Simba inahusishwa pia kumuhitaji Clatous Chama, Moses Phiri na Samuel Sikaonga
STORI: CAREEN OSCAR NA MARCO MZUMBE