×

Yanga SC Kuwafuata Taifa Jang’ombe Leo

KLABU ya Yanga inatarajia kusafiri leo Jumanne kuelekea Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi huku mchezo wao wa kwanza wakicheza Januari 5, dhidi ya Taifa Jang’ombe.

 

Yanga itasafiri huku wachezaji sita wakikosekana katika safari hiyo ambao ni Fiston Mayele, Khalid Aucho ambao wameomba ruhusa ya kwenda kwao.

 

Wachezaji wengine ni Mukoko Tonombe, Djuma Shabani na Yannick Bangala ambao wameitwa kwenye Timu ya Taifa ya DR Congo kwa ajili ya mechi ya kimataifa ya kirafiki kujiandaa na Afcon.

 

Huku kipa namba moja Djigui Diarra yeye ameitwa timu ya taifa ya Mali iliyopo kwenye mashindano ya Afcon yanayofanyika Cameroon mwezi huu.

 

Wachezaji wote waliobakia wataenda Zanzibar kwenye mashindano hayo ya maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku Yanga wakiwa ndio Mabingwa watetezi.

 

Kocha Nasreedin Nabi aliliambia Championi Jumatatu kuwa: “Mashindano ya Mapinduzi Cup yana umuhimu mkubwa sana kwetu, kwa sababu tunahitaji kuwapa nafasi wachezaji ambao hawajapata nafasi bado kwenye ligi.

 

“Lakini pia kushinda kombe hilo kwetu itakuwa ni faraja kubwa sana, kwa sababu itatuongezea kujiamini na kuendeleza heshima yetu.”

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Leave a Comment