×

Mwigulu Afafanua Matumizi ya Tsh Tril 1.3 – Video

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ametolea ufafanuzi ugawanyo wa fedha Sh trilioni 1.3 zilizokopwa na Serikali kutoka Shirika la Fedha (IMF) miezi kadhaa iliyopita.

 

Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo, Dk Nchemba amesema Serikali imetoa Sh bilioni 330 kwa ajili ya Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini ( TARURA) kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

 

Dk Nchemba amesema Sekta ya Maji imepata Sh bilioni 139.4, Sekta ya Afya ilitengewa Sh bilioni 466.8 na Sekta ya Elimu ilikuwa Sh bilioni 368.9.

 

“Kati ya fedha zilizotolewa, Sh bilioni 304 zilitengwa kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa madarasa 15,000 ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, pamoja na mabweni 50 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, hivyo kupunguza msongamano kwa wanafunzi,”amesema Dk Mwigulu Nchemba.

 

Amesema Sh bilioni 28.7 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 25 vya VETA vya Wilaya na Sh bilioni 19 ni kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo vinne vya VETA ngazi ya Mkoa ikiwemo Njombe, Simiyu, Geita na Rukwa na sekta zingine.

 

Leave a Comment