
Benki ya CRDB imewataka Watanzania kutumia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki hiyo kwa makundi mbalimbali ya wateja kufanikisha malengo waliyojiwekea katika mwaka mpya wa 2022.
Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Unachostahili ni CRDB Bank” inayolenga kutoa elimu na kuwaonyesha Watanzania fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki yao ya CRDB ikiwemo huduma za mikopo na ulipaji wa ada mbalimbali bila usumbufu.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema CRDB inatambua kuwa inawajibu wa kuwasaidia Watanzania na wadau wengine wa maendeleo nchini kutimiza malengo katika mwaka huu mpya 2022.
Pia, Nsekela akaeleza mafanikio yaliyopatikana katika huduma za Sim Banking tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2011.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema lengo la uzinduzi wa kampeni hiyo ni kutoa elimu juu ya huduma na bidhaa, kuongeza ubora wa huduma kwa wateja pamoja na kuongeza utumiaji wa bidhaa na huduma za CRDB (9:00)
Ameongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kumuweka kwanza mteja na kuwakaribisha Watanzania wote, wateja binafsi, makampuni, na taasisi kuchangamkia fursa hizo kufikia malengo yao

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda aliwashukuru Watanzania kwa kuendelea kuichagua benki hiyo kuwa mtoa huduma wao na kuwaahidi benki hiyo itaendelea kuwapa wanachostahili kupitia bidhaa na huduma bunifu.