×

Aslay: Tusisahau Kuna Kuishi

STAA mwingine mkubwa wa Bongo Fleva, Aslay isihaka anasema kuwa, watu wafanye kazi, lakini wasisahau kuna kuishi kwa sababu maisha ni mafupi.

 

Akizungumza na IJUMAA SHOWBIZ, Aslay ANASEMA kuwa, siku zote katika maisha watu huwa wanaweka jitihada zao zaidi kwenye kutafuta pesa, lakini wanasahau hata kupata muda wa kutulia sehemu nzuri na familia zao, jambo ambalo siyo zuri kiafya.

 

“Binadamu tunatakiwa tupate muda mzuri wa kupumzika na kutuliza akili zetu, siyo wakati wote unafanya kazi tu bila hata kutuliza akili, hiyo siyo nzuri kiafya ndiyo maana mimi huwa nafanya sana kazi, lakini najua kuna kuishi ndiyo maana kuna muda lazima nipumzike na familia yangu, naamini kufanya hivyo ndiyo kunanifanya nizidi kuachia hit song kwa sababu akili pia inakuwa imetulia,” anasema Aslay.

Leave a Comment