×

Man United Hawamtaki Cristiano Ronaldo

MAMBO sio mazuri ndani ya Manchester United, huku ikielezwa kuwa staa wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo awekwe
kando kwani
anagawa timu na wachezaji 11 wanatajwa kutaka kuondoka kikosi hapo.


Hii imekuja siku
chache baada ya Man United kushindwa kutamba mbele ya Wolves na kufungwa bao 1-0 ukiwa ni
mchezo wa Premier
uliopigwa Uwanja wa Old Trafford.


Taarifa zinaeleza
kuwa mambo sio mazuri ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya timu hiyo
kwa sasa.
Ripoti zinaelezwa kuwa wachezaji kama Harry Maguire, Edinson Cavani na Mason Greenwood

 

Na imeelezwa pia amekuwa kama akishawishi jambo Wareno wenzake pamoja na wale ambao wanazungumza Kireno yaani Bruno Fernandes, Diogo Dalot, Fred na Alex Telles.


Taarifa zimeenda
mbali zaidi na kueleza kuwa wachezaji wapatao 11 kwa sasa wanataka kuondoka klabuni hapo
kutokana na hali hiyo.


Hata hivyo mtoa taarifa
alinukuliwa akisema: “Mambo sio mazuri, hali haiko sawa na muda unavyoenda huenda hali ikawa mbaya ndani ya United.”


Beki wa timu hiyo,
Luke Shaw alikiri baada ya kipigo hicho kuwa: “Wachezaji hawapo pamoja na hawajitumi. Sisi wachezaji ambao tumekuwa kwa muda mrefu hapa huwa tunafahamu mambo yanakuwaje ila ile hamasa haipo tena ni kama hatupo pamoja kabisa.”

Leave a Comment