×

Waarabu Wamfuata Saido Burundi

TAARIFA zinasema kwamba, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ wamemfuata nyumbani
kwao Burundi na viongozi
wa timu moja kutoka Uarabuni kwa ajili ya mazungumzo ili kumsajili.


Saido ambaye hivi
karibuni aliondoka Tanzania kwenda Burundi kwa ajili ya mapumziko mafupi, wakati akiwa huko ndipo Waarabu hao walipomuibukia kwa nia ya kumshawishi wamsajili.

 


Nyota huyo aliyetua
Yanga dirisha dogo la msimu uliopita, mkataba wake unatarajiwa kumalizika
mwisho wa msimu huu.

 


Mtu wa karibu na mchezaji
huyo, ameliambia Spoti Xtra kwamba: “Hivi karibuni Saido akiwa kwao Burundi
alifanya kikao na mwakilishi
wa timu kutoka Uarabuni ambayo siwezi kuitaja.

 


“Anaweza kukubali dili
hilo maana lina pesa nyingi, ila kwa upande wa viongozi wa Yanga wamemwambia asubiri wakimaliza Mapinduzi wataongea naye kujadili mkataba mpya.”

 


Alipotafutwa Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema: “Kuhusu suala la Saido lazima ataongezewa mkataba.”

STORI: CAREEN OSCAR NA LEEN ESSAU, DAR

Leave a Comment