×

Yanga Yampa Ulaji Kocha Azam

MTENDAJI Mkuu waAzam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema kuwa kwa sasa hawana mpango wa
kuachana na kocha wao wa muda,
Msomalia,Abdihamid Moallin.

 

Moallin ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Somalia, alituaAzam FC kama Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha Kukuza Vipaji chaAzam (AzamAcademy) lakini alipewa kazi ya kuinoa timu ya wakubwa kwa muda baada ya kutimuliwa kwa Kocha Mkuu, George Lwandamina.

 

Juzi aliiongozaAzam FC kushinda mchezo wao wa nusu fainali wa Kombe la Mapinduzi kwa penalti 9-8 dhidi ya
Yanga na sasa watacheza fainali dhidi
ya Simba, keshoAlhamisi Uwanja wa Amaani visiwani hapa.


Akizungumza na
Championi Jumatano, Popat alisema kuwa: “Kuingia fainali kwetu ni furaha kubwa sana kwani ni muda kidogo hatukuingia, hii kwetu ni hatua kubwa.

 

“Vijana wetu wamepambana sana pamoja na benchi la ufundi, hatuoni haja ya sisi kuweza kutafuta kocha mwingine wakati kocha wetu anafanya vizuri, tutaendelea kuwa na kocha huyu huyu.”

STORI: CAREEN OSCAR, Unguja

Leave a Comment