×

Mbunge nchini Kuwait afariki wakati wa kikao cha bunge.

Kuwaiti MP Nabil al-Fadel smokes a cigar as he attends a parliament session requested by opposition MPs to grill Kuwaiti Finance Minister Mustafa al-Shamali over alleged financial and administrative irregularities in Kuwait City on May 24, 2012. AFP PHOTO/YASSER AL-ZAYYAT (Photo credit should read YASSER AL-ZAYYAT/AFP/GettyImages)Nabil al-Fadl enzi za uhai wake.

MBUNGE wa Kuwait Nabil al-Fadl (65) amefariki dunia ghafla leo baada ya kuanguka kutoka kwenye kiti chake bungeni wakati wa kikao cha bunge la nchi hiyo.

kuwait_parliamenBunge la Kuwait.

Wabunge walimzingira na kutaharuki hali iliyojitokeza bungeni humo wakati Waziri wa Afya wan chi hiyo, Dkt Ali al-Obaidi akijaribu kumtibu hadi wakati madaktari walipowasili.

Marehemu Al-Fadl — ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari alikuwa maarufu kwa kutumia jarida lake kuwaasa wabunge wenzake na hata wakati mwingine kuwakosoa.

Aidha Al-Fadl alifahamika zaidi kwa kuwakaripia waasi wa Kiislamu ambao aliwashambulia kwa maneno makali.

Wakati mmoja aliwashangaza wasomaji wake alipoitaka serikali iondoe mara moja marufuku ya uuzaji wa pombe na maeneo ya burudani.

CREDIT: Al Arabiya News Channel

Leave a Comment