
Baada ya sintofahamu ya muda mrefu , hatimaye kiungo wa Kimataifa wa Zambia, Clatous Chota Chama amewasili Nchini kujiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba SC.
Chama ambae aliachana na Simba mwishoni mwa msimu uliopita na kujiunga na RS Berkane ya Nchini Morocco, amerejea baada ya mambo kutomwendea vyema nchini Morocco.
Makamu wa Rais wa klabu ya RS Berkane ya Morocco, Majid Madrane amethibitisha rasmi kuwa Chama amerejea katika Klabu ya Simba.