
Mabiti wa kike waliokatiza masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito wamerejea shuleni ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali wa elimu ya sekondari kwa njia mbadala unaoratibiwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEMW).
Mpango huo ni Mradi wa kuimarisha ubora wa elimu sekondari (SEQUIP-AEP). Katika picha, Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Wamo Morogoro iliyopo chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Naomi Yakobo ameonekana akiwapa maelekezo ya masomo wanafunzi wakike waliokuwa wamekatisha masomo na kurejea tena kuanza masomo yao Januari 17, 2022 kupitia mpango wa elimu Sekondari kwa njia mbadala.