×

Kiungo Mnigeria Asepa Simba

KIUNGO, Udoh Utop jana Jumapili aliondoka rasmi nchini ambapo alikuja kwa ajili ya majaribio ndani ya Simba
na kurejea kwao nchini
Nigeria.


Udoh alikuja nchini
sambamba na winga mwenye uraia wa Ivory Coast, Cheick Mounkoro na Sharaf Shiboub
waliofanya majaribio na
Simba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi lakini hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kupata mkataba.


Akizungumza na
Championi Jumatatu, Udoh Utop alisema kuwa tayari ameshaondoka kurejea kwao nchini Nigeria ambapo kuna ofa nyingine amezipata, lakini kama kuna timu itakuwa ipo tayari kumsajili kutoka Tanzania yupo tayari kujiunga nayo.


“Tayari safari yangu
imeiva na leo (jana) Jumapili nitaondoka kuelekea Nigeria ambapo ni nyumbani, kuna
ofa nimepata kutoka timu
nyingine sehemu mbalimbali nakwenda kuziangalia baada ya kushindwa kusajiliwa na
Simba.


“Kuhusu Tanzania
nimependa mazingira yake na soka lake hivyo kama kutakuwa na timu yoyote kutoka Tanzania itanihitaji basi nipo tayari kujiunga nayo,” alisema kiungo huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave a Comment