
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula ametuma salamu za rambirambi kufuatia tukio la wanawake watatu kuuawa kikatili kisha miili yao kutupwa, tukio lililotokea Januari 19, 2021 katika Mtaa wa Mecco Kusini, Kata ya Mecco jijini Mwanza.
Dkt. Mabula amelaani tukio hilo na kuviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa tukio hilo kwa haraka na kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kuhusika na ukatili huo.
Aida Dokta Mabula amewataka wananchi, ndugu na jamaa wa marehemu kuwa watulivu wakati serikali na vyombo vya dola wakiendelea kushughulikia tukio hilo.