
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (kulia) amefiwa na kaka yake, aliyekuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Gerald Mpango ambaye amefariki dunia Januari 19, 2022 jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Askofu Mpango anatarajiwa kuzikwa nyumbani Kigoma na ibada ya kumuaga marehemu itafanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta Jijini Dar es Salaam, kesho Ijumaa Januari 21, 2022.
Mwili utasafirishwa kwenda Kigoma kisha kufuatiwa na Ibada ya kuaga mwili huo katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea Kasulu Kigoma.