
MSANII maarufu duniani wa RnB, Robert Sylvester Kelly ‘R. Kelly’ ameanza kutafuta mawakili wengine wa kumuwakilisha kwenye kesi yake mjini Chicago baada ya mawakili wake wawili Steve Greenberg na Michael Leonard kuomba kuondolewa kwenye kesi hiyo tangu Juni mwaka jana.
Mawakili walikuwa wakimwakilisha R. Kelly mahakamani Mjini New York kwenye kesi yake ya unyanyasaji wa kingono kwa mabinti iliyokuwa na makosa 14 ambapo iwapo atakutwa na hatia na anaweza kufungwa maisha jela.
Kwenye kesi ya mjini Chicago R Kelly anakabiliwa na makosa ya kutengeneza filamu za ngono na watoto wenye umri chini ya miaka 18, vitisho kwa mashahidi na kujaribu kununua ukimya wao. Kesi ya Chicago itaanza kusikilizwa Machi mwaka huu.