
UNAAMBIWA mpenzi mpya wa mwanamitindo maarufu duniani, Kim Kardashian aitwaye Pete Davidson ameajiri walinzi binafsi kwa mara ya kwanza baada ya kusikia Ex wake na Kim ambaye ni rapa Kanye West anataka kumdhuru kupitia wimbo wa ‘EAZY’.
Kanye alirap kwenye nyimbo zake akisema kuwa; “God saved me from that crash/ just so I can beat Pete Davidson’s a**.”
Ikiwa inaripotiwa kuwa ni utani tu ya Kanye kwenye nyimbo zake, Pete hajachukulia suala hilo kimasihara, yeye amelichukulia siriaz na kuamua kuajiri walinzi na atakuwa anatumia walinzi wa Kim K wakati wakiwa pamoja.