
RAPA maarufu duniani Sean John Combs ‘P Diddy’ ameanza kazi ya kukamilisha albamu yake mpya ambayo hapo awali aliahidi angeitoa mwezi Septemba, mwaka jana.
Albamu hiyo ya Off The Grid Vol. 1 ambayo itawapa mashabiki wa Rnb, Rap na Hiphop nafasi ya kuonja radha ya ubunifu mwingine wa P Diddy imeanza kutayarishwa na producer na music engineer wa TDE ‘MixedByAli’ katika studio yake ya Can-Am.
Hapo zamani hizi zilikuwa studio za Death Row Records walipofanyia kazi wasanii wakubwa nchini Marekani kama Dr. Dre, Snoop Dogg, na Tupac.
Diddy amekuwa kimya kwa muda mrefu hivyo mashabiki wake wammiss kwenye game ya muziki kwani amekuwa akiutendea haki.