×

Dkt. Mpango Aaga Mwili wa Kaka Yake

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango, amewaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu kaka yake Askofu Gerald Mpango leo Ijumaa, Januari 21, 2022.

Gerald Mpango alikuwa Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Western Tanganyika ambapo ibada ya kuaga mwili wake imefanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, ndugu jamaa na marafiki.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa kanisa la Anglikana, ndugu, jamaa na familia kutokana na msiba wa Askofu Mpango.

Mwili wa Askofu Mpango ambaye alifariki dunia juzi Jumatano, Januari 19, 2022 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu utasafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoani Kigoma kwa ajili ya mazishi.

 

Leave a Comment