×

Priyanka Chopra na Nick Jonas Wapata Mtoto

MREMBO Priyanka Chopra(39) na Nick Jonas(29) wapata mtoto wa kike baada ya kumuajiri mwanamke wa kuwabebea mimba yao(surrogate). Mtoto amezaliwa tarehe 15 wikiendi iliyopita.

 

Star huyo Miss World wa mwaka 2000, hivi karibuni alikuwa bize nchini Hispania na London kumalizia kushuti series yake mpya ya kipelelezi Citadel toka kwa Ruso Brothers ambayo itaoneshwa Amazon, mrembo huyo ndie mwigizaji mkuu wa series hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya kuonekana katika toleo jipya la filamu ya Matrix.

 

Priyanka alipokuwa akiulizwa kuhusu kuanzisha familia mara zote alikuwa akijibu kuwa yupo bize sana na mikataba ya kikazi ingawa akipata muda tu yeye na Nick star wa Marekani wataanzisha familia. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2018.

Leave a Comment