×

Kanye West Aungana na Nike

NI HEADLINES kutoka kwenye kiwanda cha burudani, rapa maarufu duniani, Kanye West mbioni kufanya ushirikiano wa kibiashara na Michael Jordan.

 

Aidha, Kanye anafanya mchakato wa kurudisha ushirikiano wake wa kibiashara na Kampuni ya NIKE baada ya kutengana Kibiashara kwa miaka 9.

 

NIKE ni kampuni ambayo ilimtambulisha vizuri kwenye ulimwengu wa biashara na kumuingizia fedha nyingi.

 

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, YE ameweka nembo maarufu ya bidhaa za Michael Jordan ‘Jumpman’ lakini pia aliweka Tweet ya mtoto mkubwa wa MJ, Marcus Jordan ambaye aliandika kwamba anataka kuwakutanisha YE, DJ Khaled na Michael Jordan kwa mazungumzo.

 

Mwaka 2013 Kanye West aliachana vibaya na NIKE na kisha kusaini dili na kampuni ya Adidas, dili lililokuwa na thamani ya ($10 million) zaidi ya TSh. Bilioni 22.

Leave a Comment