×

Rais Samia Ampongeza Dr. Salim Kwa Kutimiza Miaka 80

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia amepongeza Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania (1984-1985) Dr. Salim Ahmed Salim kwa kutimiza umri wa miaka 80 leo Januari 23, 2022, pia amemshukuru kwa utumishi wake kwa taifa.

“Kheri ya siku ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Dkt. Salim Ahmed Salim, mtumishi mahiri wa umma wa Watanzania, Afrika na Dunia kwa zaidi ya miongo minne. Katika siku hii adhimu ya kumbukumbu ya miaka 80 ya kuzaliwa kwako, tunakushukuru kwa utumishi uliotukuka kwa nchi yetu.” amesema Rais Samia

Leave a Comment