MCHEZO wa kombe la shirikisho la Azam Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya 32 umekamilika, kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc, mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Yanga licha ya kuwakosa nyota wake kadhaa ilionesha kandanda safi na kutengeneza nafasi za wazi huku Jesus Moloko akikosa nafasi za wazi za kufunga.

Bao pekee la Yanga limefungwa na Mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 54, Yanga imesonga mbele kwenye michuano hiyo na kutinga hatua ya 16 bora.