
UONGOZI wa Dar City umefunguka kuwa mchezo wao wa leo Jumapili dhidi ya Simba, utakuwa mkali zaidi tofauti na ile mitatu waliyocheza wapinzani wao dhidi ya Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Mbeya City.
Dar City leo Jumapili watakuwa wageni wa Simba katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho
la Azam (ASFC) unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar kuanzia saa 1:00 usiku.
Akizungumza na SpotiXtra, Rais wa Dar City, Azim Khan, alisema: “Kikosi kiliingia kambini Jumanne wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huu dhidi ya Simba.
“Tunawaheshimu Simba ni timu kubwa na lolote litatokea kwani mpira ni dakika 90, kama uongozi tumerekebisha baadhi ya matatizo ambayo yalikuwepo kwenye timu. “Utakuwa ni mchezo wa tofauti na ushindani mkubwa kwani ni wa mtoano, utakuwa mchezo mkali zaidi na tunaamini tutapata ushindi.”
STORI: LEEN ESSAU, Dar es Salaam