×

50 Cent amshitaki Rick Ross kwa kutumia beat ya wimbo wake

50-Cent1

Curtis James Jackson III ’50 Cent’.

Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, Curtis James Jackson III ’50 Cent’ amemfungulia mashitaka Rapa
William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’ kwa kurap kupitia beat ya wimbo wake wa “In Da Club” wakati akiipigia promo albamu yake mpya ya Black Market.

Rick Ross Mastermind Press photo 2014

William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’.

50 amefungua shauri hilo Connecticut, Marekani na katika viambatanisho vya kesi hiyo anasema
wimbo wake umetumiwa na Rick Ross katika mixtape yake iitwayo ‘Renzel Remixes’ bila ruhusa yake na ameitumia katika kuitangaza albamu yake mpya.

50 na Ross wana bifu la siku nyingi na kuna kipindi 50 alilipishwa dola milioni 7 kwa kosa la
kuachia kanda ya video ya ngono ambayo alikuwemo pia mpenzi wa Ross.

50 anataka Ross amlipe zaidi ya Dola milioni 2 kwa kosa hilo la kutumia beat ya wimbo wake.

Rick Ross – In Da Club
 

 

Leave a Comment