×

Pablo Aitisha Kikao ghafla Juzi Simba

UNAAMBIWA muda mfupi baada ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City, Kocha Mkuu
wa Simba raia wa Hispania, Pablo
Franco, ameitisha kikao ghafla Juzi Simba iliibuka na ushindi huo mnono katika mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports uliochezwa Uwanja wa Mkapa,
Dar.


Kwa siku za karibuni, Simba
imekuwa haina matokeo mazuri katika ligi kuu hali inayotishia kulikosa taji wanalolitetea kutokana na kuachwa pointi kumi na vinara Yanga baada ya timu zote kucheza mechi 13.


Chanzo chetu kutoka Simba,
kimeliambia Spoti Xtra kuwa, baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Dar City, Kocha Pablo ambaye hakuwepo kwenye benchi kutokana na kufungiwa mechi tatu, aligoma kuzungumza lolote na wachezaji.
“Ushindi wetu wa jana (juzi
Jumapili), umeongeza morali kwa wachezaji kuanza kuona mwelekeo katika mechi zijazo tukianza na Prisons.


“Kutokana na ushindi huo na
mchezo ulio mbele yetu, ndiyo kisa cha Kocha Pablo kuwataka wachezaji wawahi kambini leo (jana Jumatatu), ili kupata muda wa kukaa kikao na uongozi kabla ya kuanza mazoezini kujiandaa
kuwakabili Prisons,” kilisema
chanzo hicho.


Alipotafutwa Meneja wa Habari
na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Kikao kilipangwa kufanyika baadaya mazoezi ya jioni (jana Jumatatu) ambapo ni kawaida ya kocha na wachezaji kuzungumza kukumbushana
mambo.”


Katika mechi tatu zilizopita za
Ligi Kuu Bara, Simba imekuwa na matokeo yasiyoridhisha ambapo imekusanya alama moja kati ya tisa kutokana na kupata suluhu dhidi ya Mtibwa Sugar na kupoteza mbele ya Mbeya City na Kagera

Sugar.

NA~MUSA MATEJA NA WILBERT MOLAND

Leave a Comment