×

Mrembo wa ‘Utu’ ya Kiba Afunguka Pesa Anayolipwa

MREMBO maarufu kwa kuuza sura kwenye nyimbo za wasanii Bongo, Nana Dollz ambaye ameing’arisha Video ya Utu ya King Kiba amefunguka kisa cha pesa anacholipwa ili auze nyago kwenye video ya msanii.

Nana anasema kuwa, kiwango cha pesa ambacho analipwa kwenye ishu ya kuwa video vixen kwenye video ya msanii ni shilingi milioni tatu kwani hiyo ndiyo kazi yake.

Hadi jana, Video ya Utu inashika namba moja kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki ikiwemo YouTube.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave a Comment