×

Dube: Nimerudi Kuwafungia Mabao Azam FC

BAADA ya kupitia kipindi kigumu cha kuandamwa na majeraha, hatimaye straika wa Azam FC, Prince Dube,
amesema kuwa kwa sasa yupo fiti,
anataka kupambana na kuifungia mabao mengi timu yake.


Dube amesema msimu uliopita
alipishana na kiatu cha ufungaji bora kwa sababu alikuwa anaumia mara kwa mara, lakini kwa sasa yupo fiti na anarudi akiwa na nguvu kubwa uwanjani.


Akizungumzia hali yake kiafya na
mwenendo wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu, Dube alisema kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa timu nyingi na ushindani umeongezeka, ila kwa kuwa amepona na kuwa fiti, atafanya kile mashabiki wake wanataka.


“Msimu niliuanza vibaya kutokana
na majeraha. Niliumia sana kwa sababu malengo yalikuwa ni kuisaidia timu
ila nashukuru nimerejea na nipo tayari
kwa hilo,” alisema.

 

Stori: Issa Liponda, Dar es Salaam

BARAKA MPENJA Achambua SIMBA vs TZ PRISONS, UTATA wa PENALTY, KIWANGO cha CHAMA..

Leave a Comment