×

Wema: Hata Nikifa, Nyota Yangu Itang’aa

MTU anaweza kuwa staa kwenye eneo lake kwa muda f’lani, lakini akatokea mwingine kwenye mazingira yaleyale akawika huku baadhi wakiamini nyota yake itazimika; kama siyo leo, basi ni kesho!


Katika tasnia ya burudani
Bongo kuna mastaa wenye nyota kali kuliko wengine na wakati mwingine, uwezo wa sanaa yao unawabeba huku wengine wakiwa na viwango vya kawaida kabisa, lakini wanabebwa na nyota zao.

 

Mifano ipo mingi ambapo kuna wasanii wapo miaka nenda-rudi kwenye sanaa, lakini wapo vilevile, lakini kuna wengine wanaingia kama chipukizi na wanampita na kumuacha palepale.


Kuna wasanii ni wa muda
mrefu, lakini hawachuji, hata kama wakipotea kwa muda, lakini wakirudi na kufanya kazi moja tu, wanarudi juu tena kama vile alikuwa ulingoni siku zote.


WEMA AWA TALK OF THE
TOWN

Hiyo ni kwa sababu moja tu; nyota kung’aa kwani wapo wasanii wengi wa aina hiyo Bongo, lakini kiboko yao ni mwigizaji Wema Isaac Sepetu kwa sasa mashabiki wake wanapenda kumuita Last Born wa Taifa; yaani Kitindamimba au Kiziwanda wa Taifa!


Wema aliyekuwa kimya kwa
muda, ghafla tu wiki hii amekuwa talk of the town (gumzo la mji) baada ya kudai kudhalilishwa na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Aristote.


Katika moja ya intavyu zake,
Aristote alidai Wema hawezi kumfikia mwigizaji mwenzake, Irene Uwoya kwa sababu hana gari na si mzuri huku akimsifia Uwoya kwamba ni mzuri na anaendesha gari aina ya Range Rover.


Ishu hiyo imemrejesha Wema
kwenye kilele cha umaarufu kutokana na namna anavyotetewa ambapo siri ya nyota yake kung’ara imeeleza.


WEMA: NITAZEEKA, KUFA NA
NYOTA YANGU

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA, Wema anasema kuwa, ataendelea kung’ara hata kama akizeeka na kuwa kikongwe kisha kuaga dunia.


Wema anasema kuwa, nyota
yake itaendelea kung’aa siku zote wala haitafifia kama baadhi ya watu wanavyotamani iwe kwani amezaliwa nayo na atazikwa nayo na akiwa kaburini bado ataendelea kuzungumzwa.


“Hata kama watu wataichafua
kiasi gani, nyota yangu itaendelea kung’aa hadi nitakapokuwa mzee. Nitakuwa ni bibi mwenye mvuto na hata nikifa bado watu watataka kunizungumzia na kusikiliza hadithi zangu,” anasema Wema.


Hata hivyo, Wema anamshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia nyota hiyo ambayo inawezekana kuna watu wanatamani izimike wakati wowote, jambo ambalo haliwezekani leo wala kesho na kwa kuwa alitoka nayo tumboni kwa mama yake, Miriam Sepetu.

 

NYOTA YA WEMA NI LIBRA

Wema ambaye amezaliwa Septemba 28, 1990, nyota yake ni mizani au libra.


Kwa mujibu wa Mnajimu
na Mtaalam wa Nyota nchini Tanzania, Maalim Hassan, Wema anaangukia kwenye nyota hiyo ambayo ni nyota ya utendaji, ulaini wa mambo, yenye amani, kupenda uzuri na sifa njema na yenye kung’ara katika jamii kwa muda wote.

 

“Wenye nyota ya mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa jumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.


“Ni watu wastaarabu, wenye
adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana,” anasema na kuongeza; “Wenye nyota hii watu wakiwaangalia mara nyingi, huwaona kuwa ni watu wa muhimu sana katika jamii na huwa hawasahauliki.”


WEMA ANG’ARA MIAKA 16

Wema alitambulika kwa kofia ya Miss Tanzania mwaka 2006/07 ambapo ushindi wake ulikuwa wa kishindo kikuu akiwa kwenye ushindani mkubwa na Jokate Mwegelo, Lisa Jensen na Irene Uwoya. Hawa walikuwa warembo moto katika Miss Tanzania ya mwaka huo.


Hata hivyo, Wema alikuja kupata
heshima kubwa zaidi baada ya marehemu Steven Kanumba kumuingiza kwenye tasnia ya Bongo Movies.


Nyota ya Wema ilianza kuonekana
tangu aliposhiriki filamu yake ya kwanza kabisa, A Point of No Return akiwa na Kanumba.


Baada ya hapo, Wema ameendelea
kufanya vizuri kwenye filamu za Kibongo huku akitajwa kama miongoni mwa mastaa 10 Bora waliofanya vizuri zaidi kwenye tasnia hiyo kwa muda wote. Ukitazama Filamu ya DJ Ben, White Maria, 14 Days, Red Valentine utaelewa kwa nini anapewa sifa hizo.


Nje ya sanaa, Wema ametokea
kuwa na mashabiki wengi wanaomfuata kwenye kurasa zake katika mitandao ya kijamii akiwa nao milioni 9.4 kwenye Instagram pekee.


Pia ana wafuasi wake (Team
Wema) ambao wamejenga umoja wa kumsapoti kwenye kila jambo hata kama akifanya jambo baya, wamekuwa mstari wa mbele kumtetea.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment