×

Dully: Darasa Nimemlea

NGULI wa muziki wa bongo fleva, Dully Sykes ameweka wazi mchango wake alioutoa kwenye muziki huo ikiwemo kulea vipaji vya wasanii kadhaa ambao wamegeuka nyota wakubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva akiwemo rapa  Sheriff Thabeet ‘Darasa’.

 

Kupitia mahojiano yake na chombo kimoja cha habari nchini, Dully amesema; “Mimi huwa ni muongeaji lakini sio mtu ambaye huwa nataka credit zangu, hivi ulikuwa unajua kama Darassa amepita Misifas Camp?

“Sipendi kujipakulia minyama kwasababu kiukweli katika wakongwe ambao wametunza wasanii ambao leo wanafanya vizuri, Mimi Sijawahi Kujizungumzia.

“Lakini kama nikitaka kujizungumzia, kina Darasa wote wamepitia mikononi mwangu na ni wakubwa, sasa hivi ni wa kimataifa, hawa na wasanii wengine sitaki kuwataja hapa wote.

 

“So huwa sina desturi ya kuzungumzia hivyo vitu na havina faida, Kama umeumbwa mwanaume na una akili huwezi ukazungumza kwamba flani nimewasaidia, haipendezi utasubiri wenyewe watasema,” alisema Dully.

Leave a Comment