
Mjumbe wa kamati kuu ya ACT Wazalendo Hamad Masoud ambaye alikuwa mgombea nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi uliomaliza wiki iliyopita ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho.
Kiongozi huyo ametumia maneno ya mafumbo katika taarifa yake rasmi ya kuondoka ACT kwa kusema “wanaosema yeye wa nini wengine wanauliza watampata lini”
Hamad Masoud alishindwa kwenye uchaguzi wa kumsaka mwenyekiti mpya wa Chama hicho na Juma Duni Haji katika uchaguzi uliolalamikiwa na waliokuwa wafuasi wa kambi yake katika uchaguzi huo wa kumrithi Hayati Maalim Seif Sharif kwenye kiti hicho.