×

Tanasha: Sijali Diamond Kumuoa Zuchu

SUPASTAA wa Tanzania, Diamond Platnumz na msanii wake wa WCB, Zuchu wamekuwa wakitrendi tangu
Desemba, mwaka jana wakidaiwa
ni wapenzi kutokana na ishara mbalimbali wanazozionesha.


Madai kwamba, wawili hao
wanatoka kimapenzi yalichochewa na kitendo cha Diamond kumtoa Zuchu ‘auti’ usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar.

 

Watu kibao wa Wasafi wakiongozwa na Mama Dangote, Romy Jons, Rayvanny na ‘machawa’ ndiyo wakaanza kuimba mapenzi ya Diamond na Zuchu.

 

Hata alipoulizwa Bi Khadija; mama wa Zuchu, naye akasema hakuna ubaya wakioana kwani siyo ndugu wa tumbo moja.

Madai hayo yalikwenda mbali zaidi ikielezwa kwamba, Diamond amepanga kumuoa Zuchu siku ya Valentine
Februari 14, 2022.

Hata hivyo, stori zilibadilika wiki iliyopita baada ya Zuchu kukana kutoka kimapenzi na Diamond zaidi ya uhusiano wa kikazi.


Muda wote wakati sakata
hilo likifukuta, ma-baby mama wa Diamond, Zari The Boss Lady, Hamisa Mobeto na Tanasha walikuwa kimya.

Hata hivo, baada ya kusumbuliwa ma maoni mengi juu ya Diamond kutaka kumuoa Zuchu, Tanasha amevunja ukimya akisema; “Sijali…” Badala yake anasema kuwa, kwa upande wake yeye ameelekeza nguvu zake kwenye sanaa yake ya muziki.

STORI: STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave a Comment