
IKIWA ni siku chache baada ya kutangazwa kushuka kwa mapatao yake, wiki hii kuna mvutano mkubwa unaendelea kati ya kampuni ya Meta (Facebook) na Umoja wa Nchi za Ulaya.
Sheria mpya ya Umoja wa Ulaya (GDPR Data Rules), inazitaka kampuni zinazokusanya data za watumiaji wa nchi za Ulaya, kuhifadhi na kuchakata data za watumiaji wa Ulaya kwenye server zilizopo Ulaya na kutumia mfumo maalum wa kusafirisha data nje ya Ulaya.
Meta imesema itachukua uamuzi wa kuzima huduma zake za Facebook na Instagram kwa watumiaji wa nchi za Ulaya. Imesema ni vigumu data zote kuchakatwa na kuhifadhiwa Ulaya.
Endapo kama itashindikana, itafuta huduma zake ambazo zinatumia server za Marekani na app ambazo zipo hatarini kufungiwa ni Instagram na Facebook.
Viongozi wa nchi za Ulaya wameshikilia msimamo wao na wiki hii mkuu wa Kidigitali wa EU amesema ni makosa kwa Facebook kutishia kuondoa huduma zake kwa sababu Umoja wa Nchi za Ulaya upo tayari kuzifuta Instagram na Facebook.