×

Shamsa: Tulitendwa, Lakini Tumeibuka Mashujaa

MWANAMAMA mwingine mkali kwenye kamera za Bongo Movies, Shamsa Ford anasema kuwa, yeye na staa mwenzake, Faiza Ally walitendwa na wanaume ambao wamezaa nao, lakini hali hiyo imewafanya wakawa wanawake mashujaa, wenye maendeleo na ndoto kubwa.

 

Akistorisha na Gazeti la IJUMAA, Shamsa anasema kuwa, yeye na Faiza wakizungumza huwa
wanasikilizana mno kwa sababu
wamepitia machungu ya kulea wenyewe watoto wao tena kwa shida, lakini wamesimama imara.


“Mwanamke yeyote ambaye
amepitia matatizo ya kulea mtoto wake mwenyewe, anaweza kujua nazungumza nini na ndivyo ilivyokuwa kwangu mimi na Faiza ambaye tunaweza tukazungumza lugha moja na tukaelewana.

 

Pia ni watu tunaofarijiana sana kwa kweli na tutatoboa tu tukiwa wenyewe hivihivi bila mwanaume pembeni na sasa tumeibuka mashujaa,” anasema shamsa ambaye analea mtoto wake, Terry mwenyewe bila baba yake Dick.


Kwa upande wake, Faiza
anasema kuwa, anapenda siku zote kumchukulia mfano Shamsa kwa sababu amepitia hali hiyo na mpaka sasa anapitia, lakini hatetereki

Leave a Comment