×

Harmonize: Jux ni Brother, Sisi ni Ndugu

NI HEADLINES za mastaa wa Bongo Fleva, Jux na Harmonize zinaendelea kwenye tasnia ya muziki wa Bongo na entertainment kwa ujumla.

 

Moja ya maswali yaliyoulizwa leo kwenye press ya Harmonize ni kuhusu malalamiko ya Jux kuwekwa kwenye orodha ya watakao-perform kwenye Afro East Carnival bila makubaliano kufikiwa inavyotakiwa ambapo haya ndio majibu ya Harmonize.

“Jux ni Brother amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu, mimi nimekuwa shabiki yake napenda muziki wake, hizo miss-understanding zilitokea kutoka kwa Management, watakaa kulimaliza, halikuwa na haja ya kwenda kwenye media.

 

“Japo naheshimu uwepo wa media lakini sio kila kinachotokea kinatakiwa kuwa public maana kukiwa na mikwaruzano wakati mwingine inawakatisha tamaa wale wenye Taasisi zinazo-support muziki, Serikali na wadau tutaonekana wasanii hatujielewi.

“Nirudie kusema sisi ni ndugu hatuwezi kugombana, sisi ni wamoja ni Watanzania, tusitengeneze mikwaruzano, nitahakikisha sitogombana na kaka zangu,” amesema Harmonize. 

Leave a Comment