×

Baba Levo: Hakuna Mtu Atabaki Konde Gang

MSANII wa Bongo Fleva ambaye Baba Levo amedai hakuna mtu ambaye atabaki katika Lebel ya Konde Gang inayomilikwa na Harmonize huku akidai kuwa hata Mwijaku ameanza kutuma meseji akiomba kazi Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

 

Baba Levo ambaye ni ‘Chawa’ wa Diamond amesema; “Ni ngumu kupinga ukweli, kama mtu ana mtusi Diamond kutokana na anayofanya, kuna muda hata ukajitazama kwenye kioo utajigundua wewe ni mwehu.”

Haya yote yamekuja baada ya trending ya msanii H. Baba kumpost Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram, wakati inafahamika wazi kuwa ni mpinzani wake.

 

Lakini kwa Upande wa DC wa Insta, Mwijaku amedai H. Baba hajawahi kuwa member wa Konde Gang, yule ni shabiki na msanii kama wasanii wengine, akimtolea mfano Timbulo. Lakini pia Mwijaku amesisitiza kuwa Konde Gang itabaki kuwa Konde Gang na wasanii wake wale wale ikiwa imara.

Leave a Comment