×

Nabi aukwepa mtego wa Simba

WAKATI Simba SC wakiingia kwenye mtego wa kudondosha pointi pale Manungu dhidi ya Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, ameshtuka na kusema, ana mbinu kali za kuhakikisha wakienda hapo, basi watarudi Dar na pointi zote tatu.


Kauli ya Nabi imekuja
wakati timu Mtibwa Sugar na Yanga zikitarajiwa kuvaana Februari 23, mwaka huu ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.


Januari 22, mwaka huu,
ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza Mtibwa ikicheza na Simba kwenye Uwanja wa Manungu baada ya kupita zaidi ya miaka 15, na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa suluhu.


Kabla ya kuanza kwa
mchezo ambapo siku hiyo mvua kubwa ilinyesha, Simba waliulalamikia uwanja huo kwa kile kilichoelezwa hauna ubora sehemu ya kuchezea, lakini mwisho wa mechi ikapigwa.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Nabi alisema anafahamu mashabiki wana hofu ya kupata matokeo mazuri kutokana na miundombinu ya uwanja huo ambao ulisababisha watani wao, Simba waambulie suluhu.


Nabi alisema kwake hana
hofu, kwani alishawahi kupata matokeo mazuri katika viwanja vibovu msimu huu na uliopita.


“Mimi kama kocha
ninafanya maandalizi ya kuwaandaa vijana wangu siku mbili hadi tatu kabla ya mchezo husika kulingana na aina ya uwanja ninaokwenda kuutumia.


“Hivyo sasa maandalizi
ninayaelekeza dhidi ya Mtibwa ambao uwanja wao wanaoutumia miundombinu yao mibaya.


“Nitafanya maandalizi
kutokana na uwanja huo tutakaokwenda kuutumia, siyo mchezo wangu wa kwanza kutumia uwanja mbovu, msimu huu nimepata ushindi kwenye viwanja vibovu, hivyo sina hofu katika hilo, tutaenda kupata ushindi hukohuko kwao,” alisema Nabi.

WILBERT MOLANDI,DAR

Leave a Comment