×

Mtibwa Waitaka Yanga Manungu

UONGOZI wa Klabu ya Mtibwa Sugar, umeweka wazi  kuwa, mchezo wao dhidi ya Yanga utafanyika Uwanja wa Manungu uliopo mkoani Morogoro na wala hawatauhamisha kwenda popote.


Februari 23, mwaka huu,
Mtibwa watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Akizungumza na
Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: “Watu wanazusha kuwa mechi sijui itafanyika Tabora, lakini nataka niwaambie kuwa mechi ipo palepale katika uwanja wetu wa Manungu.


“Sisi tunaitaka Yanga ije
hapa Manungu, tumejipanga vizuri kuwakabili. “Kwa namna yoyote ile tutapata ushindi, huko nyuma tumepoteza mechi, lakini kwa Yanga tutapambana kushinda.”

MARYAM SALMIN, DAR ES SALAAM

SIMBA WAWAFUATA WANIGER KIMAFIA, MORRISON NDANI, KISA SIMBA, NABI AONGEZA DOZI YANGA…

Leave a Comment