×

Mwamnyeto: Tunabeba Ubingwa ASFC

BEKI wa kati wa Yanga ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto, amesema safari hii wanahitaji kufika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kuwa mabingwa.


Yanga juzi
Jumanne walifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa
mabao 2-1 dhidi
ya Biashara United katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumz na Spoti Xtra, Mwamnyeto alisema, malengo yao msimu huu ni kuhakikisha
wanatwaa
ubingwa wa michuano hiyo.

 

“Tunatakiwa kufika fainali ili tuwe mabingwa wa a michuano hii, akili zetu na malengo yetu yapo katika michuano hii na lazima tuhakikishe tunatimiza.


“Wapinzani wanatakiwa
kujipanga kwani hata sisi tayari tumeshajipanga kucheza na timu yoyote itakayojitokeza
mbele yetu, hakuna jambo
ambalo lisilowezekana, ni kujituma tu na kuwa na nia ya kuwa mabingwa na sisi tunayo
nia,” alisema nahodha huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, DAR ES SALAAM

USIPIME! YANGA Wapiga TIZI la KIBABE Kuelekea KUWAVAA Mtibwa Sugar UWANJA wa MANUNGU..

Leave a Comment