
KIUNGO wa Simba, Clatous Chama, amesema kuwa kwa sasa amefikia kwenye kiwango chake ambacho alikuwa anahitaji kukifikia.
Chama alisema wakati anaondoka Simba ni tofauti na alivyorejea tena kwa sababu alikuta kuna mabadiliko kidogo lakini kwa sasa yupo sawa na anaweza kuipambania timu kwa asilimia 100.
Akizungumzia maendeleo yake ndani ya timu tangu aliporejea, Chama amesema kitu kizuri kwake ni kwamba amekutana na wachezaji wengi walewale ambao aliwaacha ndiyo maana haijamchukua muda kurejea kwenye ubora wake.
“Wakati nimekuja hapa, nilikuwa bado nipo chini kwenye suala la utimamu wa mwili wangu, namshukuru Mungu kwa sasa kila kitu kipo sawa na naweza kuipambania timu kwa asilimia 100.
“Ndiyo, kuna mabadiliko machache kwenye benchi la ufunid lakini kitu kizuri ni kwamba wachezaji wengi ni walewale ambao niliwaacha wakati naondoka, hiyo imenisaidia sana,” alisema.
Chama alirejea tena Simba baada ya kuondoka miezi sita iliyopita na kujiunga na RS Berkane ya Morocco. Tangu
arejee amefunga mabao manne ikiwemo hat trick kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Ruvu Shooting.