×

Mapokezi Ya Rais Samia Akitokea Ubelgiji (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anawasili nchini kutoka Ubelgiji, Leo Februari 20, 2022 baada ya ziara yake nchini Ufaransa na baadae Ubelgiji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022 mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi ya Ufaransa na Ubelgiji.
Sehemu ya Wananchi wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022.   

Leave a Comment