×

Mourinho Aiponda PSG vs Madrid

JOSE Mourinho, Kocha wa AS Roma, amesema hakufurahishwa na mchezao kati ya PSG dhidi ya Real Madrid, huku akidai kwamba hajamisi kuwa ndani ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Mourinho kwa sasa anainoa Roma ambayo haipo kwenye michuano hiyo, huku ikishiriki Europa Conference League.


Jumanne ya wiki hii,
PSG iliifunga Real Madrid bao 1-0 ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.


“Nimekuwa kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya nikisimamia mechi zaidi ya 150, hivyo sina presha, kwa sasa siwezi
kuanza kulia eti
sababu kwa timu yangu ipo Europa au Conference League.

“Sijafuatilia mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ila sikupenda mechi ile ya PSG na Real Madrid
hata kidogo, walau
mechi ya Inter Milan na Liverpool ilikuwa ni bora na nzuri,” alisema Mourinho ambaye aliwahi kuinoa Real Madrid kuanzia 2010 hadi 2013.

Leave a Comment