×

Al- Shabab Yatumia Bil. 55 Kununua Silaha

KUNDI la al-Shabab mwaka 2021 lilitumia dola milioni 24(£18m) sawa na TZS bilioni 55.5 kununua silaha hii ni kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Hiraal lenye makao yake mjini Mogadishu.
 
Ripoti imefafanua kuwa kundi hilo lenya mfungamano na al-Qaeda lina mapato ya TZS bilioni 416.5 kwa mwaka, linayokusanya pia kupitia kodi katika maeneo ya Somalia inayoyakalia.
 
 
Ripoti hiyo , inasema kundi hilo linatumia mbinu mbalimbali kupata silaha, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa moja kwa moja kutoka soko la ndani, na kutoka kwa wafanyabiashara wa silaha walio na kandarasi ya kununua na kusambaza silaha kutoka nje ya nchi, hasa Yemen.
 

Leave a Comment