
MMOJA wa mashabiki wa Yanga, mwenye asili ya Kimasai anaefahamika kwa jina la Mauya mkazi wa Dakawa, amemzawadia ng’ombe mzima Mshambuliaji wa Timu ya Yanga na mfungaji wa goli la Pili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar Fiston Mayele.
Mayele amepewa Zawadi hiyo Leo Februari 23 katika Dimba la Manungu Mkoani Morogoro baada ya kufunga goli lililoisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar.