×

Papa Francis Atangaza Machi 2 Siku Ya Kuiombea Ukraine

 

Kufuatia kile kinachoendelea baina ya Urusi na #Ukraine, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema hatari ya vita ilmesababisha maumivu makali moyoni mwake.

 

Ametoa wito kwa watu wote kutumia siku ya Machi 2, 2022 ambayo ni Jumatano ya Majivu, kufunga na kuiombea Ukraine.

 

Ripoti zinaonesha tayari #Russia imeanza kuishambulia Ukraine. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema watashinda vita hivyo.

Leave a Comment