×

Ukraine Yaomba Msaada Kukabiliana na Urusi

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa ombi jingine kwa washirika wa nchi za Magharibi kuisaidia Ukraine na kukomesha mashambulizi ya kikatili ya Urusi.

 

“Leo asubuhi tunalinda taifa letu peke yetu. Kama jana, majeshi yenye nguvu zaidi duniani yanatazama kutoka mbali,” Zelensky alisema katika hotuba yake kwa taifa.

“Je, Urusi ilishawishika na vikwazo vya jana? Tunasikia katika anga yetu na kuona kwenye ardhi yetu kwamba hii haitoshi.”

Kiongozi wa Ukraine amethibitisha mashambulio mengi ya makombora yaliyoripotiwa alfajiri ya leo.

Zelensky alisema mashambulizi hayo yalianza saa kumi asubuhi kwa saa za huko Ijumaa ameongeza kuwa mashambulizi ya Urusi yalilenga maeneo ya kijeshi na ya kiraia,  Urusi hapo awali ilisema hailengi raia.

Leave a Comment