×

Zelensky: Hatutazungumza na Urusi Nchini Belarus

Urusi inasema wajumbe wake wamewasili nchini Belarus kwa mazungumzo na Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekataa ombi hilo, akisema mazungumzo ya Minsk yangewezekana ikiwa Urusi isingeishambulia Ukraine kutoka nchini Belarus na kueleza kuwa anaacha mlango wazi kwa mazungumzo katika maeneo mengine.

Alisema: “Kama hakungekuwa na hatua kali kutoka eneo lenu, tungeweza kuzungumza Minsk… miji mingine inaweza kutumika kama mahali pa mazungumzo.

“Bila shaka tunataka amani, tunataka kukutana, tunataka vita viishe. Warsaw, Bratislava, Budapest, Istanbul, Baku – tumewapa Warusi.

“Jiji lingine lolote litatufaa katika nchi, ambayo makombora yake hayarushwi dhidi yetu. Hii ndiyo njia pekee ya mazungumzo yanayoweza kuwa ya ukweli na yanayoweza kumaliza vita.”

Leave a Comment