
Takriban watu 21 wameuawa na wengine 112 kujeruhiwa katika shambulio la makombora katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv, meya wa jiji hilo amesema.
Hata hivyo, gavana wa Tawala za Jimbo la Kharkiv amesema mashambulizi yote ya Urusi yalijibiwa na maeneo kushikiliwa licha ya mashambulizi makubwa ya Kharkiv siku ya Jumanne.
Gavana Oleh Synegubov amesema: “Adui yetu, Urusi amepata hasara kubwa”.
Inafahamika kuwa wanajeshi wa Urusi waliingia katika maeneo ya Kaskazini Mashariki na Kaskazini mwa mji huo huku pia mji huo ukishambuliwa kwa ndege zenye kutumia silaha kutoka kwenye anga.