×

Kiiza: Huyu Mayele Atafunga Sana Yanga

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba ambaye hivi sasa anacheza Kagera Sugar, Mganda, Hamis Kiiza
‘Diego’amemuangalia straika waYanga,
Mkongomani, Fiston Mayele na kutamka kuwa jamaa anajua huku akimtabiria makubwa katika timu hiyo.


Kiiza aliyewahi kuichezeaYanga kabla ya
kwenda Simba, alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yaYanga dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja
wa Mkapa, Dar es Salaam.


Mchezo huo ulimalizika kwaYanga kushinda
mabao 3-0 yakifungwa na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’na Mayele aliyepachika mawili.


Akizungumza na Championi Jumatano,
Kiiza ambaye aliwafunga Simba katika mchezo wa ligi, alisema kuwa kwa aina ya uchezaji na mfumo ambao wanautumiaYanga, mshambuliaji huyo atafunga mabao mengi
msimu huu.


Kiiza alisema kuwaYanga mashambulizi yao
wanayafanya kutokea pembeni wakiwatumia mabeki wa pembeni na mawinga kupiga krosi ambazo ndiyo zinamrahisishia Mayele kufunga mabao.


Aliongeza kuwa uzuri wachezaji wote
wa Yanga wanamjua vizuri Mayele, hivyo wanatumia mipira ya krosi katika kumpa mipira hiyo ambayo inazaa mabao.


“Kwa aina ya uchezaji na kimbinu
wanayotumia wachezaji wenzake kumchezesha Mayele, basi namtabiria kufanya mengi mazuri katika msimu huu ikiwemo kutwaa ufungaji bora.


“Yanga mashambulizi yao wanayatumia
kupitia pembeni kwa maana ya kupiga krosi ambazo zote wanampigia Mayele, ni kitu ambacho wanaonekana kukifanyia kazi mazoezi.


“Mabao yote aliyotufunga Mayele yametokea
pembeni moja la krosi na lingine la faulo iliyotokea pembeni ambayo yote yakifungwa kwa kichwa,” alisema Kiiza.

STORI: WILBERT MOLANDI | CHAMPIONI JUMATANO

RAIS WA UKRAINE UVUMILIVU WAMSHINDA, AJITOKEZA HADHARANI KUOMBA MSAADA – “URUSI INATAKA KUTUUA WOTE”

Leave a Comment