×

Unyama: Baba Amuua Mwanae Kwa Kumrushia Shoka – Video

Polisi Mkoani Kagera wanamshikilia Anderson Clemence (35) Mkazi wa Kitongoji cha Ihema, Kijiji cha Kafunjo Wilayani Karagwe Mkoani Kagera kwa kumuua Mtoto wake Hansen Anderson mwenye umri wa miezi minne kwa kumpiga na shoka kichwani.

“Chanzo cha mauaji ni ugomvi wa Kifamilia kati ya Baba huyo na Mkewe Renatha Anderson ambapo Baba wa Marehemu (Mtuhumiwa) alirusha shoka kwa lengo la kumkata Mke wake na Mkewe alikwepa likampata Mtoto kichwani na akafariki papohapo”

“Kiini cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika”

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment